• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kutafutia vijana ajira nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2019-12-02 20:53:55
    Serikali ya Kenya kwa kushirikiana na sekta binafsi zimeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha vijana waliohitimua wanatafutiwa ajira nje ya nchi.

    Akizungumza baada ya kuzindua karakana za kisasa Mamlaka ya Kitaifa ya Mafunzo ya Viwanda (NITA) mjini Mombasa jana, Waziri wa Leba ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha,Ukur Yattani,alisema serikali inashirikiana na maajenti na wameweka mopango ya kuwasafirisha vijana wanaopata ujuzi kutoka vyuo anuwai vya ufundi nchini Kenya wanapata kazi nchi za ng'ambo.

    Bw Yatani alisema serikali imewekeza fedha nyingi kuhakikisha vijana wote wanapata ujuzi na vyeti ambavyo vinakubalika kote duniani.

    Baadhi ya nchi ambazo serikali inanuia kupeleka vijana kufanya kazi mbalimbali ni pamoja na Saudi Arabia ,Qatar, na Milki ya Falme za Kiarabu (UAE).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako