• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabadiliko ya hali ya tabianchi yachangia ongezeko la magonjwa ya mlipuko

    (GMT+08:00) 2019-12-03 08:40:29

    Mamlaka za afya nchini Kenya zimesema mshituko unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi kama vile ukame na mafuriko, umechochea ongezeko la magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza na kuleta changamoto kubwa kwa vituo vya afya kwenye maeneo yenye watu wenye mapato ya chini.

    Waziri wa afya wa Kenya Bibi Sicily Kariuki, amesema jamii kwenye maeneo ya vijijini na maeneo ya mabanda mijini, yamekuwa yakikumbwa na magonjwa ya kuambukiza ambayo yanatokana na kuongezeka kwa joto. Bibi Kariuki amesema hayo mjini Nairobi kwenye ufunguzi wa mkutano wa afya, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, uliohudhuriwa na watunga sera na wanasayansi zaidi ya 300, wakijadili uhusiano kati ya ongezeko la joto duniani na kuongezeka kwa magonjwa ya kitropiki nchini Kenya.

    Amesema madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kama vile mafuriko, yamesababisha ongezeko la magonjwa makali kama Malaria, Homa ya Dengue, Kipindupindu na homa ya matumbo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako