Mfuko wa Msaada wa Dharura wa Umoja wa Mataifa umetoa dola za kimarekani milioni tatu kuwasaidia wahanga wa mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Kenya. Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema fedha hizo zitauruhusu Umoja huo na mashirika mengine ya kibinadamu kutoa chakula cha dharura, uungaji mkono wa kimaisha, kambi na huduma za afya kwa walioathiriwa zaidi. Fedha hizo pia zitatumiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi ya kunywa na kuhimiza kampeni ya kujikinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |