Shirika la Masuala ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi ya kikatili dhidi ya wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu katika eneo la Maban nchini Sudan Kusini, na kutaka sheria ifuate mkondo wake dhidi ya wahalifu. Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Sudan Kusini Bw. Alain Noudehou ametahadharisha kuwa vitendo vya kimabavu dhidi ya wafanyakazi hao havikubaliki kabisa na vinatakiwa kusimamishwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |