Ufaransa imefanya hafla kwenye uwanja wa Les Invalide mjini Paris kutoa heshima kwa wanajeshi 13 waliokufa kwenye ajali ya helikopta nchini Mali wiki moja iliyopita. Hii ni idadi kubwa ya wanajeshi wa Ufaransa kufariki kwa siku tangu nchi hiyo iingie Mali 2013 kupambana na ugaidi. Habari zinasema usiku wa tarehe 25, helikopta mbili za Kifaransa ziligongana zilipokuwa zinasafiri chini kwa chini kuwaunga mkono wanajeshi waliokuwa ardhini wakipambana na wanamgambo wa huko.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |