• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Iran yakaribisha pendekezo la kupunguza mvutano wa kikanda

  (GMT+08:00) 2019-12-03 09:55:01

  Shirika la habari la IRNA la Iran limeripoti kuwa waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema Iran inakaribisha pendekezo lolote la kusaidia kupunguza mivutano katika kanda ya Mashariki ya Kati. Bw. Zarif amesema alipokutana na mwenzake wa Oman Yusufu bin Abdullah mjini Tehran, kuwa Iran inatarajia kufanya mazungumzo na nchi zote za kanda hiyo. Ameongeza kuwa pendekezo la amani la Hormuz la Iran linalenga kuleta amani, utulivu na neema kwa nchi za Ghuba na kuanzisha mahusiano ya kirafiki kati ya nchi hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako