• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • ISOKA: Tanzania Bara kufungua dimba na ndugu zao, Zanzibar kwenye michuano ya CECAFA Challenge

  (GMT+08:00) 2019-12-03 10:15:34

  Tanzania Bara itafungua dimba na ndugu zao, Zanzibar Jumapili kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayotaraiwa kuanza Desemba 7 hadi 19 mjini Kampala nchini Uganda. Baada ya kufungua dimba na Zanzibar Heroes, Kilimanjaro Stars, mabingwa wa 1975, 1994 na 2010 watarejea uwanjani Desemba 10 kumenyana na Kenya kabla ya kukamilisha mechi za Kundi C kwa kumenyana na Djibouti Desemba 12. Zanzibar wao baada ya kupambana na Tanzania Bara Jumapili, watarejea uwanjani Desemba 10 kumenyana na Djibouti kabla ya kukamilisha mechi za kundi lao kwa kukipiga na Kenya Desemba 12. Kundi A linaundwa na wenyeji, Uganda, Burundi, Ethiopia na Eritrea, wakati Kundi B linaundwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan, Sudan Kusini na Somalia. Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitaingia Robo Fainali zikiungana na mbili nyingine zitakazomaliza na wastani mzuri katika nafasi ya tatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako