Liverpool wameingia kwenye kipindi cha mwezi Desemba wakiwa mbele kwa tofauti ya pointi 11 dhidi ya wapinzani wao wakubwa kwenye mbio za ubingwa wa Premier, Manchester City wakiwa na nafasi kubwa zaidi ya kuutwaa msimu huu, lakini Kocha wa City, Pep Guardiola amedai bado nao wana nafasi. Liverpool ina pointi 40 kileleni huku Man City wakiwa na pointi 29, katika historia ya Premier hizo ni pointi nyingi zaidi kihistoria baada ya mechi 14, na timu zote mbili ambazo awali zilifikisha pointi hizo ndani ya mechi hizo zilitwaa ubingwa, ambazo ni Tottenham 1961-62 na Man City 2017-18. Liverpool juzi walifanikiwa kuwachapa Brighton mabao 2-1 kwenye mchezo ambao walipata pigo baada ya kipa wao Alisson Becker kupewa kadi nyekundu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |