Timu ya mpira wa kikapu ya Rwanda energy Group REG inalenga kushinda mashindano ya mwaka huu ya kabla ya msimu yaliyopangwa kufanyika Disemba 5 hadi 15. Ijumaa iliyopita REG ilishinda kombe la Agaciro Basketball baada ya kuigaragaza Patriots kwa alama 61-50 kwenye hatua ya fainali. Makala ya mwaka huu itafanyika katika ukumbi wa Amahoro Stadium na Kigali Arena. REG na IPRC-Huye ni mabingwa watetezi kwa wanaume na wanawake mtawalia. Mashindano hayo yatashirikisha timu 16 kwa upande wa wanawake na wanaume.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |