• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kushiriki kwenye mchakato wa pande nyingi juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

    (GMT+08:00) 2019-12-03 17:14:58

    Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa umefunguliwa jana mjini Madrid, Hispania.

    Akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu mkuu wa idara ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika wizara ya mazingira ya kiikolojia ya China Bw. Lu Xinming amesema, China itashiriki kikamilifu kwenye mchakato wa pande nyingi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Amesema China inazingatia mambo manne muhimu, ambayo ni pande zote zinatakiwa kuhimiza mazungumzo juu ya masuala yanayobaki kwenye utekelezaji wa Makubaliano ya Paris, China inataka nchi zilizoendelea kuzipatia nchi zinazoendelea msaada zaidi wa fedha, ili kuzisaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia China inataka kujumuisha utekelezaji wa ahadi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kote duniani kabla ya mwaka 2020, na kutafuta ufumbuzi wa suala hilo, na pia pande zote zinapaswa kupinga kithabiti hatua za upande mmoja za aina tofauti, na kulinda mamlaka ya utaratibu wa pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako