United waweka historia ya miaka 31
(GMT+08:00) 2019-12-03 18:52:29
Timu ya Manchester United ya Uingereza imeandika historia mpya msimu huu ya kufanya vibaya ambapo haijawahi kutokea kwa kipindi cha miaka 31 kwenye Ligi Kuu England. Mwishoni mwa wiki iliyopita timu hiyo ilikuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Old Trafford na kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Aston Villa na kuufanya kuwa mchezo wa sita msimu huu kwenye michuano hii kutoka sare. Mbali na kutoka sare kwa michezo sita, lakini imekubali kichapo cha michezo minne na kushinda michezo minne katika michezo 14 waliocheza msimu huu. Hii haijawahi kutokea kwa timu hiyo katika historia yake tangu msimu wa 1988-89 wakiwa wamecheza michezo kama hiyo. Sasa Manchester United imeachwa kwa pointi 22 dhidi ya vinara wa Ligi hiyo Liverpool.