• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahasibu wa Afrika kukutana Kigali

    (GMT+08:00) 2019-12-03 19:43:31
    Zaidi ya wahasibu 1000 kutoka Afrika watakutana mjini Kigali kuanzia Desemba 9 kujadili miongoni mwa mambo mengine mwenendo wa mabadiliko ya sekta ya fedha.

    Mkutano huo wa Chama cha Wahasibu wa Afrika pia utajadili fursa mpya za biashara, kuimarisha utenda kazi, kujiandaa kwa ajili ya hatari za kibiashara na kufikiria upya mifumo ya kibiashara.

    Mkurugenzi wa chama hicho kanda Kusini mwa Jangwa la Sahara ya Jamil Ampomah, amesema hali ya sasa ya mabadiliko duniani inahitaji mashirika ya kitaalam kuunda uhusiano na kubadilishana uzoefu.

    Mkutano huo pia unafanyika wakati bado kuna uhaba wa wahasibu nchini Rwanda hali ambayo inaweza kuhatarisha usimamizi wa fedha.

    Na Nchini Mauritius, kwa kila watu 525 nchini, mmoja ni mhasibu, nchini Uingereza, kwa kila watu 222 mtu mmoja ni mhasibu, huko Australia, ni mmoja katika kila watu 160 na Singapore ni mmoja kati ya watu 190.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako