• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali kufanya mabadiliko katika sekta ya kilimo

  (GMT+08:00) 2019-12-03 19:44:10
  Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo inakusudia kufanya mabadiliko katika sekta ya kilimo kwa kutunga sera na sheria kwa ajili ya kuyalinda maeneo ardhi ya kilimo ili yasitumike kwa mipango mingine kama ya makazi.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga kwenye hafla ya kuhitimisha mradi wa ubia kwa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika, chini ya Jangwa la Sahara unaotekelezwa kwenye nchi 10 ambapo kwa Tanzania mradi huo unatekelezwa wilayani Mvomero, Kilosa na Kilombero.

  Amesema maeneo mengi ya kilimo yamegeuzwa kuwa makazi na kufanya maeneo ya kilimo kupungua wakati idadi ya watu wanaingia katika kushiriki kilimo ikiwa inaongezeka kwa kasi na hivyo kuhatarisha kupunguza uzalishaji wa chakula.

  Waziri Hasunga amesema Serikali itaanza kuratibu mchakato wa kutengeneza sera na sheria ya kulinda maeneo ya kilimo ili kuyafanya yaweze kuendelea kuongeza uzalishaji kupitia kilimo kwa kuwa mahitaji ya chakula nchini bado ni makubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako