• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uwekezaji Same watengewa ekari 9

  (GMT+08:00) 2019-12-03 19:44:30
  Halmashauri ya Wilaya ya Same, imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari tisa katika Kata ya Gavao Saweni, kwa ajili ya kupisha mradi mkubwa wa uwekezaji wa viwanda vidogo.

  Taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule inaeleza kuwa eneo hilo ni mahususi kwa ajili ya kutekeleza shughuli za viwanda na zingine za kiuchumi ili kutoa ajira kwa makundi ya vijana.

  Alisema sekta ya viwanda inapewa kipaumbele kwa sasa kwa sababu ya nafasi kubwa iliyonayo katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuongeza pato la taifa.

  Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya alisema viwanda hivyo vinachangia kuongeza ajira, soko la bidhaa za kilimo kupitia malighafi na mzunguko wenye sura pana katika kukuza uchumi wa nchi.

  Hivi karibuni, Mkurungenzi wa Maendeleo ya Teknolojia na Uendelezaji Viwanda wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Mhandisi Emmanuel Saiguran, alikaririwa akisema uanzishaji wa viwanda vidogo utasaidia uchumi kukua na kutoa ajira kwa wingi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako