• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali kusaidia vijana kupata kazi nje ya nchi

  (GMT+08:00) 2019-12-03 19:44:51
  Serikali ya Kenya kwa ushirikiano na sekta ya kibinafsi zimeweka mikakati kabambe ya kuwatafutia vijana kazi katika mataifa ya ng'ambo.

  Waziri wa Leba ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha, Ukur Yatani, alisema serikali imepiga msasa maajenti na kuweka mipango ya kusafirisha vijana wote wanaopata ujuzi katika vyuo vya ufundi anuwai nchini kufanya kazi ng'ambo.

  Bw Yatani alisema serikali imewekeza fedha nyingi kuhakikisha vijana wote wanapata ujuzi na vyeti ambavyo vinakubalika kote duniani.

  Akiongeza mjini Mombasa baada ya kuzindua karakana za kisasa katika National Industrial Training Authority (NITA), zilizojengwa kwa msaada kutoka serikali ya Korea kwa gharama ya zaidi ya Sh300 milioni, Bw Yatani alisema wanawasiliana na maafisa wa serikali katika nchi mbali mbali kuunganisha vijana waliopata ujuzi mbalimbali wapate ajira katika nchi hizo.

  Baadhi ya nchi ambazo serikali inanuia kupeleka vijana kufanya kazi mbalimbali ni pamoja na Qatar, Saudi Arabia na Milki ya Uarabuni (UAE).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako