• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utekelezaji wa makubaliano ya Paris na utoaji wa fedha ni maswala muhimu kwa China katika mkutano wa tabia nchi

  (GMT+08:00) 2019-12-04 08:42:57

  Kutatua maswala yanayohusiana na utekelezaji wa makubaliano ya Paris ya mwaka 2015, na kutafuta njia bora za kutafuta fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ni baadhi ya maswala makubwa yatakayofuatiliwa na ujumbe wa China kwenye mkutano wa umoja wa mataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi unaofanyika huko Madrid, Hispania.

  Ofisa mwandamizi anayeshughulikia mabadiliko ya hali ya hewa katika wizara ya Ikolojia na mazingira ya China Bw. Lu Xinming, amesema jambo la kwanza wanalotaka kuhimiza ni kukamilisha mazungumzo kwenye maswala yaliyobaki ya utekelezaji wa makubaliano ya Paris, na kuweka msingi wa utekelezaji wa dunia wa makubaliano ya Paris.

  Amesema changamoto kubwa kwa sasa ni nchi zinazoendelea zinahitaji fedha ili kufikia malengo ya kupunguza viwango vya utoaji wa hewa zinazosababisha ongezeko la joto, na nchi zilizoendelea zinaweza kuonyesha mshikamano kwa kutoa fedha zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako