• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maeneo 18 ya biashara huria ya China yazidi kuboresha mazingira ya biashara

    (GMT+08:00) 2019-12-04 18:37:13

    China imetoa waraka hivi karibuni kuwa, kuanzia Desemba Mosi, maeneo 18 ya biashara huria nchini China yameanza majaribio ya kutenganisha leseni ya biashara na hati ya uendeshaji, ili kupunguza mchakato wa ukaguzi na uidhinishaji. Maofisa wanaohusika wameeleza kuwa, baada ya kukamilika kwa majaribio hayo, sera hiyo itaenezwa kote nchini.

    Nchini China, leseni na hati ni funguo mbili kwa makampuni kuingia kwenye soko. Awali, idara za usimamizi ziliweka mchakato wa ukaguzi na uidhinishaji kabla ya kuandikishwa kwa makampuni kwenye idara ya viwanda na biashara, na kuweka masharti mengi kwa makini. Mwaka 2015, eneo la biashara huria la Shanghai lilitangulia kufanya mageuzi kuhusu kutenganisha leseni ya biashara na hati ya uendeshaji nchini China, na kurahisisha kwa kiasi kikubwa mchakato wa ukaguzi. Ukweli umeonesha kuwa, mageuzi hayo yamepunguza kwa ufanisi gharama za biashara za kimuundo, na kuboresha mazingira ya biashara.

    Naibu mkurugenzi wa Idara kuu ya usimamizi ya soko la China Bw. Tang Jun anasema:

    "Mambo yote yanayohusu idhini ya uendeshaji wa biashara ya makampuni yatafanyiwa mageuzi na kuubadilisha ukaguzi kuwa kuweka kumbukumbu, na kuboresha utoaji wa huduma za ukaguzi na uidhinishaji."

    Hivi karibuni, Benki ya Dunia imetoa ripoti ya mazingira ya biashara ya mwaka 2020. Ripoti hiyo imeonesha kuwa, hali ya kuanzishwa kwa biashara nchini China imeshika nafasi ya 27 kati ya makundi 190 ya kiuchumi duniani. Lakini suala la "kuruhusiwa kuingia kwenye soko ila kutoruhusiwa kufanya biashara" bado halijatatuliwa kwa kimsingi. Bw. Tang Jun anasema:

    "Lengo la mageuzi hayo ni kutatua suala hilo. Kuzidi kupunguza masharti ya kuidhinisha makampuni kufanya biashara, ili kuyawezesha makampuni yaanzishe biashara kwa urahisi zaidi na kupata maendeleo makubwa zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako