• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga kithabiti Marekani kupitisha mswada kuhusu sera ya haki za binadamu ya wauygur ya mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-12-04 19:00:21

    Makala iliyotolewa na Shirika Kuu ya Utangazaji la China (CMG) imesema China inapinga vikali kitendo cha baraza la chini la bunge la Marekani ambalo jana lilipitisha mswada kuhusu sera ya haki za binadamu ya wauygur ya mwaka 2019, ambao umetoa taarifa zisizo sahihi juu ya hali ya haki za binadamu mkoani Xinjiang na juhudi za China katika kupambana na watu wenye itikadi kali na ugaidi.

    Muswada huo pia umeshambulia sera ya serikali ya China kuhusu Xinjiang, kitendo ambacho kimekwenda kinyume cha sheria ya kimataifa na kanuni ya kimsingi ya mahusiano ya kimataifa, na ni kitendo cha kuingilia mambo ya ndani ya China, na serikali na watu wa China wana nia imara ya kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya nchi.

    Makala hiyo imesema, mambo ya Xinjiang ni mambo ya ndani ya China, na maendeleo ya mkoa huo hayawezi kufutwa na baadhi ya watu wa Marekani. Marekani lazima ijirekebishe, kuzuia mswada huo uwe sheria, na kusimamisha kuingilia mambo ya ndani ya China kwa kutumia suala la Xinjiang, ili kuepuka kuharibu zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako