• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajerumani waingiwa na kiwewe kuwekeza Afrika Mashariki.

    (GMT+08:00) 2019-12-04 19:18:07
    Matumaini ya kufanya biashara Afrika Mashariki kwa Kampuni za Kijerumani yamefifia, hali ambayo huenda ikaathiri uwekezaji wa kigenu kwenye mataifa haya. Kwenye utafiti uliofanywa na ujumbe maalum wa kibiashara Afrika Mashariki kutoka Ujerumani, matarajio ya wamiliki wa biashara wa kampuni za Kijerumaniyamedorora kwa kiasi kikubwa kwa miezi 12 iliyopita.

    Taifa la Tanzania lipo chini zaidi kwa asilimia 25, likidaiwa kuwa na vikwazo vingi vya kuendesha biashara, Watanzania kupendelea sana kampuni zao za nyumbani, ukosefu wa ujuzi kwa waajiriwa na ununuzi finyu.

    Rwanda ilipewa asilimia 60. Kulingana na utafiti, ni rahisi kwa kampuni za Kijerumani kuendesha biashara zao nchini Rwanda ikilinganishwa na mataifa mengine Afrika Mashariki. Hata hivyo, tatizo kuu na Rwanda ni uchache wa waajiriwa wenye ujuzi unaohitajika na ukosefu wa soko.

    Kenya ina asilimia 62 huku Uganda ikiwa na asilimia 43.

    Taifa la Ethiopia lina asilimia ya juu zaidi, ambayo ni 75. Kudorora kwa matumaini ya wawekezaji kutoka Ujerumani huenda kukaathiri kwa kiwango fulani uchumi wa mataifa ya ukanda huu wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako