• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utafiti mafuta, gesi wafikia pazuri.

  (GMT+08:00) 2019-12-04 19:18:26
  Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, imesema matokeo ya utafiti wa nishati ya mafuta na gesi bado haujakamilika na uko katika hatua za mwisho za kusoma mistari ya picha zilizopigwa.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Nishati, Salama Aboud Talib, alisema hayo jana wakati akitoa ufafanuzi kuhusu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotaka kupewa taarifa za matokeo ya utafiti wa mafuta na gesi.

  Salama alisema mkataba wa mgawanyo wa mafuta na gesi ulitiwa saini Novemba 23, mwaka jana, na baada ya hapo kazi ya utafiti ilianza mapema.

  Alisema kampuni ya Rakgas kutoka Rasilkhema iliipa kazi ya kufanya utafiti kampuni ya BGC kutoka China kwa kupiga picha za angani na kufanya mitetemo ardhini na baharini.

  Kwa mujibu wa waziri, kazi inayofanyika ambayo inahitaji uangalizi wa hali ya juu, ni kutafsiri mistari ya picha zilizopigwa katika maeneo mbali mbali vikiwemo vitalu vya mafuta vilivyoko Unguja na Pemba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako