• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda, Zimbabwe na Tanzania zawashauri Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vikubwa vya utalii vilivyopo barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-12-04 19:19:44
    Wadau katika sekta ya utalii kutoka nchi za Uganda, Zimbabwe na Tanzania wamewashauri Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vikubwa vya utalii vilivyopo barani Afrika, kama njia mojawapo ya kuunga mkono utalii wa ndani.

    Wamesema kuna haja makundi ya vijana katika nchi zao kutumia vivutio hivyo kama njia ya kuhamasisha umoja wa Afrika na ushirikiano katika nyanja muhimu za maendeleo ikiwamo fursa ya utalii.

    Wakizungumza baada ya safari ya siku sita ya kuelekea kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, wajumbe watatu kutoka nchi za Uganda, Tz na Zimbabwe, walisema lichaya mlima huo kuwa katika orodha ya maajabu saba duniani, na kuwa mlima mrefu kupita yote barani Afrika, bado vijana wengi hawajautembelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako