• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa vyombo vya habari duniani wafanyika hapa Beijing

  (GMT+08:00) 2019-12-04 19:24:26

  Mkutano wa vyombo vya habari duniani ambao mada yake ni "Vyombo vya habari na Teknolojia", na Baraza la 9 la video la dunia umefanyika leo hapa Beijing.

  Wakati huohuo, jopo la washauri mabingwa la CGTN limeanzishwa, likiwa na lengo la kuhimiza ushirikiano kati ya washauri mabingwa duniani, kujenga jukwaa wazi la mawasiliano ya kimataifa, kukuza mawasiliano kati ya tamaduni tofauti na kutoa sauti tofauti kwa dunia.

  Mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Shen Haixiong amesema, Shirika hilo linajitahidi kushikilia nafasi ya maendeleo ya teknolojia na kutoa mkakati wa maendeleo ya 5G, 4K na 8K, na akili bandia (AI) ili kuhimiza vyombo vya habari vipya kwa teknolojia mpya. Amesema anatumai jopo la washauri mabingwa la CGTN linaweza kuwa jukwaa la kimataifa la mazungumzo na ushirikiano wa wataalamu, na kuwahimiza wataalamu wengi wa China kuingia katika jukwaa hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako