• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MASUMBWI: Bondia Anthony Joshua asema ushindi wake dhidi ya Andy Ruiz hautoshangaza kwani atashinda tu

  (GMT+08:00) 2019-12-05 08:25:37

  Bondia Anthony Joshua amesema ushindi wake dhidi ya Andy Ruiz hautoshangaza kwasababu anatarajia kushinda katika pambano lake la Jumamosi nchini Saudi Arabia. Joshua ameonekana akiwa amepunguza uzito zaidi nchini Saudi Arabia kuliko alivyokuwa wakati alipopigana na Ruiz jijini New York Juni mosi. Katika pambano la kwanza lililozaa mechi ya marudiano Ruiz alimdondosha mara nne Joshua kabla ya pambano kumalizika katika raundi ya saba, lakini Joshua amesema mara hii itakuwa tofauti kwa sababu lengo lake ni kuchukua mikanda yake ya IBF, WBA na WBO. Katika mapambano yake 16, Joshua amepigana na kushinda dhidi ya mabondia bora kama Wladimir Klitschko na Alexander Povetkin. Wakati huohuo Mpuerto Rico Luis Pabon ametajwa kuwa mwamuzi wa pambano hilo la ubingwa wa dunia. Pia majaji watatu watakaoamua pambano hilo ni Mwingereza Steve Gray, Mmarekani Glenn Feldman na Mcanada Benoit Roussel. Pambano hilo lililopewa jina la 'The Clash on the Dunes' litafanyika kwenye Uwanja wa Diriyah na kuchukua mashabiki 15,000, hapo Jumamosi usiku. Waandalizi wa pambano hilo nchini Saudia wamewekeza kitita cha $40m (£33m) kuandaa pigano hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako