• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema mchakato wa kupambana na malaria unaendelea polepole

    (GMT+08:00) 2019-12-05 09:44:27

    Shirika la Afya Duniani WHO imetoa ripoti kuwa, ingawa mafanikio makubwa yamepatikana katika kupambana na malaria miaka 10 iliyopita, lakini katika miaka ya hivi haribun kasi ya kupungua kwa ugonjwa huo imeshuka, na malengo muhimu huenda yasitimizwe.

    Ripoti hiyo imesema kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2015, nchi nyingi zilikaribia kutokomeza ugonjwa huo, lakini katika miaka ya hivi karibuni, kasi ya kupunguza kiwango cha maambukizi imeshuka. Mwaka jana kulikuwa na maambukizi mapya milioni 228 ya ugonjwa huo, lakini idadi hiyo kwa mwaka 2017 ilikuwa milioni 231.

    Ripoti hiyo pia imesema, mchakato wa kupunguza vifo kutokana na ugonjwa huo pia umekuwa wa polepole. Kiwango cha vifo kwa mwaka 2016 hadi mwaka 2018 kiko chini ikilinganishwa na mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako