• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaidhinisha ujenzi wa maeneo mapya ya ngazi ya taifa ya teknolojia na ya hali ya juu ya kilimo

  (GMT+08:00) 2019-12-05 16:57:08

  Hivi karibuni Baraza la serikali la China limeidhimisha ujenzi wa maeneo mawili mapya ya kielelezo ya teknolojia mpya na ya hali ya juu ya kilimo yaliyoko Jin Zhong Mkoa wa Shanxi na Nanjing mkoa wa Jiangsu. Hadi sasa, idadi ya maeneo ya kielelezo ya aina hiyo ya ngazi ya taifa imefikia manne, hivyo kuonesha kuwa juhudi za China katika kutafuta njia ya maendeleo ya kilimo kwa msukumo wa uvumbuzi zinazidi kuharakishwa.

  Kwa mujibu wa agizo la Baraza la serikali la China, maeneo hayo mawili mapya ya kielelezo ya teknolojia mpya na ya hali ya juu ya kilimo kila moja lina viwanda vyake vikuu. Lile la Jinzhong la mkoa wa Shanxi litashughulikia zaidi mambo ya kilimo kisichochafua mazingira, na kuchukua utengenezaji wa chakula kisicho kikuu kuwa viwanda vikuu. Katibu wa kamati ya mji wa Jinzhong Bw. Zhao Jianping anasema:

  "Wakulima wa eneo la Jinzhong wametafuta na kukuza teknolojia mbalimbali za kilimo bila ya umwagiliaji, na kuweka mazingira mzuri ya kuongeza ushawishi, uwezo wa uvumbuzi na ushindani wa kilimo bila ya umwagiliaji."

  Viwanda vikuu vya Eneo lingine la kielelezo mkoa wa Jiangsu ni kilimo cha ikolojia, ambalo linalenga kujengwa kuwa eneo la kielelezo la ushirikiano wa sayansi na teknolojia ya kilimo la kimataifa, kituo cha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya kilimo cha eneo la mtiririko wa Mto Changjiang, na eneo la kielelezo cha kustawisha vijiji kwa njia ya sayansi na teknolojia. Kaimu meya wa mji wa Nanjing Bibi Han Liming anasema:

  "Hivi sasa eneo hilo limeanzisha ushirikiano na vyuo vikuu maarufu duniani ikiwemo Chuo Kikuu cha Wageningen cha Uholanzi, na Chuo Kikuu cha Hebrew cha Israel, katika siku za baadaye litahimiza ujenzi wa mashirika ya utafiti yenye kiwango cha juu zaidi duniani."

  Naibu waziri wa sayansi na teknolojia nchini China Bw. Xu Nanping amesema, anatumaini maeneo hayo ya kielelezo yataongoza sekta ya kilimo ya China kuelekea kwenye njia ya maendeleo kwa uvumbuzi, ili kuelekeza mageuzi ya kimuundo ya kilimo. Pia amesisitiza kuwa inatakiwa kujenga mazingira mazuri ya uvumbuzi na kuanzisha biashara, ili kuyawezesha makampuni mengi ya uvumbuzi kupata maendeleo, na kujumuisha raslimali za dunia nzima kujenga vizuri maeneo hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako