• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Lengo la Marekani juu ya suala la Xinjiang hayatafanikiwa

  (GMT+08:00) 2019-12-05 19:50:47

  Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetoa makala kuhusu hatua ya Baraza la chini la bunge la Marekani kupitisha mswada kuhusu sera ya haki za binadamu ya wauygur ya mwaka 2019, na kusema kitendo hicho kinaingilia mambo ya ndani ya China bila ya msingi wowote, kikiwa na lengo la kuharibu ustawi na utulivu wa mkoa wa Xinjiang, na kuharibu mchakato wa kustawisha tena taifa la China.

  Makala hiyo imesema, suala la Xinjiang si suala la kikabila, kidini au haki za binadamu, bali ni suala la kupambana na ugaidi na kupinga kufarakanisha taifa. Serikali ya mkoa wa Xinjiang imepata mafanikio katika kupambana na ugaidi na itikadi kali, hivyo kupata njia mpya ya kupambana na ugaidi inayokubaliwa na jumuiya ya kimataifa.

  Pia makala hiyo imesema China inataka Marekani iache fikra za vita baridi, kuzuia muswada huo kuwa sheria, na kusimamisha kuingilia mambo ya ndani ya China kwa kutumia suala la Xinjiang.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako