• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuondoa nguvu zote zinazozuia maendeleo yake

  (GMT+08:00) 2019-12-05 19:51:11

  Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Le Yucheng leo amehudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 20 ya kuanzishwa kwa ofisi ya mjumbe maalumu ya wizara ya mambo ya nje ya China iliyoko mkoa wa utawala maalumu wa Macao.

  Akihutubia hafla hiyo, Bw. Le amesema nguvu kadhaa za kimataifa hazitaki kuona maendeleo ya China na mafanikio ya sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", ambazo zinazusha vurugu juu ya masuala ya Hong Kong, Xinjiang na Taiwan. Amesema muswada wa haki ya binadamu na demokrasia ya Hong Kong na muswada kuhusu sera ya haki za binadamu ya Wauygur ya mwaka 2019 iliyotolewa na Marekani ni kuingilia mambo ya ndani ya China, na China inapinga vikali kitendo hicho.

  Amesisitiza kuwa China ya leo ina matumaini na nguvu ya kuondoa usumbufu wa nje, watu wote wa China watavunja njama zote za kuzuia mshikamano na maendeleo ya China, watalinda kithabiti sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" pamoja na mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako