• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mganda Kuwakilisha Afrika Mashariki Mashindano Ya Pool Kimataifa Nchini China

  (GMT+08:00) 2019-12-05 20:50:17

  Amos Ndyagumanawe kutoka Uganda amefuzu kushiriki mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Pool yajulikanayo kama "Chinese 8 Ball WeMasters Championship 2020" yanayotarajiwa kufanyika mjini Qinhuangdao nchini China kuanzia Januari 3 – 8, mwaka ujao na kushirikisha mataifa 42. Amos alifuzu nafasi hiyo katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Whisky River, Nairobi nchini Kenya katika mashindano yaliyoshirikisha nchi za Tanzania, Uganda na wenyeji Kenya, ambapo alizawadiwa pesa taslimu za Kenya shilingi 200,000, saa ya ukutani ya kisasa inayoashiria mchezo wa Pool, Ticket ya Ndege ya kwenda na kurudi nchini China pamoja na huduma zote za chakula na malazi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako