• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar kuwekeza katika uvuvi wa bahari kuu

    (GMT+08:00) 2019-12-05 20:55:58
    Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kujikita katika uwekezaji wa uvuvi wa bahari kuu pamoja na kujenga viwanda vya kuchakata mazao ya baharini ili yalete tija katika mabadiliko ya uchumi wa bahari.

    Haya ni kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda ,Hassan Khamis Hafidh,wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Tumbe,Omar Seif Abeid ,aliyetaka kujua serikali imejipanga vipi katika kuwawezesha wavuvi kuvua bahari kuu.

    Hafidh alizitaja juhudi zilizoanza kuchukuliwa na serikali ikiwamo kununua boti ya uvuvi ya Sehewa 2 ambayo itakuwa inavua kwenye bahari kuu.

    Alisema uvuvi wa bahari kuu umechelewa kuanza kufanyiwa kazi na kutoa huduma kufuatia kukosekana kwa vyombo vya uvuvi vyenye uwezo wa kuyafikia maeneo hayo.

    Aidha alisema mikakati ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuhakikisha wavuvi wanavua katika maeneo ya bahari kuu ambayo bado hawajavuliwa kwa ajili ya kupata tija kiuchumi na maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako