• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Huduma za treni jijini Nairobi zasitishwa kutokana na mafuriko

  (GMT+08:00) 2019-12-05 20:56:17
  Huduma za treni kote jijini Nairobi zimesitishwa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia alhamisi.

  Kampuni ya Reli ya Kenya ilichapisha taarifa kwenye mitandao yake ya kijamii ikisema kuwa imesitisha huduma za treni kutoka makao makuu ya treni za Nairobi na vituo vya Ruiru,Kikuyu,Syokimau,Embakasi na Kikuyu kutokana na mafuriko katika maeneo kadhaa ya barabara za reli za maeneo hayo.

  Kwenye taarifa hiyo,kampuni ya reli iliwaomba radhi wateja na kuwataka kutafuta njia mbadala kufika wanakoelekea.

  Aidha kampuni ya reli ya Kenya imesema inashughulika kurejesha huduma hizo haraka iwezekanavyo.

  Wateja wengi walitatizika baada ya kufika katika vituo mbalimbali vya kuabiri garimoshi mapema alhamisi,na hatimaye kupokea taarifa kuwa huduma hizo zitakosa baada ya kusubiri kwa muda mrefu.

  Baadhi yao pia walilazimika kulipa nauli za juu za usafiri wa magari ya umma maarufu matatu,zilizotumia fursa hiyo kuongeza nauli wanazotoza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako