• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Everton yamtimua Marco Silva kama kocha wake baada ya kuifunda kwa miezi 18

  (GMT+08:00) 2019-12-06 08:45:12

  Klabu ya Everton imetangaza rasmi kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Marco Silva ikiwa ni miezi 18 tu kuwa na klabu hiyo kufuatia kipigo cha 5-2 walichokipata dhidi ya Liverpool ugenini katika uwanja wa Anfield usiku wa December 4 2019. Uongozi wa Everton umechukua maamuzi hayo kufuatia kuona timu yao inazidi kuyumba hadi sasa ikiwa imecheza micheza 15 ya EPL wakiishia kushika nafasi ya 18 katika Ligi Kuu England inayoshirikisha jumla ya timu 20. Katika michezo hiyo 15 Everton ikiwa chini ya utawala wa kocha Marco Silva wameshinda game 4, sare mechi 2 na wamepoteza mechi 9 wakiwa na point 11. Mmoja wa mrithi wake anaripotiwa kuwa mwenzake Vitor Pereira wa Shanghai SIPG. Kwa sasa mshambuliaji wa zamani Duncan Ferguson amekuwa msimamizi wa muda na ataiogoza klabu hiyo dhidi ya Chelsea siku Jumamosi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako