• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Surua iliwaua watu 140,000 mwaka jana, wengi wakiwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano

  (GMT+08:00) 2019-12-06 09:15:12

  Watu zaidi ya 140,000 walifariki dunia kote duniani kutokana na ugonjwa wa surua mwaka jana, wengi wao wakiwa ni watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wakati matukio ya surua yanaongezeka kwa kasi. Kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni yaliyotolewa na Shirika la Afya Duniani na Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Maradhi cha Marekani CDC, sehemu iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa huo ni eneo la Afrika kusini mwa Sahara, ambapo watoto wengi wanakosa chanjo. Mwaka jana, nchi zenye maambukizi zaidi ya surua zilikuwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Liberia, Madagascar, Somalia na Ukraine, na zimechangia karibu nusu ya maambukizi yote ya surua duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako