Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema jaribio lolote la kuzuia China kujiendeleza hakika litashindwa. Akikutana na watu wa sekta mbalimbali wa Korea Kusini mjini Seoul, Bw. Wang amesema China imepata maendeleo makubwa kwa kuwa imefuata njia sahihi ya maendeleo ya ujamaa wenye umaalumu wa kichina. Hata hivyo baadhi ya nchi hazifurahii mafanikio ya China na kujaribu kukwamisha maendeleo ya China, hali hii inatokana na upendeleo ya kiitikadi au ujeuri wa nchi hizo zenye nguvu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |