• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yatoa wito wa msaada wa dharura wa dola za kimarekani milioni 180 kuisaidia Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2019-12-06 17:20:37

    Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetoa wito wa msaada wa dharura wa dola za kimarekani milioni 180 ili kuwasaidia wakimbizi wa ndani wanawake na watoto wa nchini Sudan Kusini.

    Mwakilishi wa UNICEF nchini Sudan Kusini Mohamed Ag Ayoga amesema, watoto milioni 4.1 nchini humo wanahitaji msaada wa dharura, na kwamba mgogoro wa kisiasa unaoendelea na ukosefu wa huduma za muhimu unawazuia wakimbizi hao kurejea makwao na kuanza upya maisha yao.

    Amesema watoto wanaokulia nchini Sudan Kusini hawawezi kulaumiwa kwa hali ya nchi hiyo, hata hivyo, wao ndio wanalipia gharama kubwa zaidi kwa maisha yao ya baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako