• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa Mipango ya maendeleo ya mafungamano ya Eneo la mtiririko wa Mto Changjiang

    (GMT+08:00) 2019-12-06 17:27:24

    Hivi karibuni, China ilitoa Mwongozo wa Mipango ya maendeleo ya mafungamano ya Eneo la mtiririko wa Mto Changjiang. Maofisa wengi wa China wameeleza kuwa, ni alama muhimu ya eneo la mtiririko wa Mto Changjiang kupata maendeleo yenye sifa ya juu ya mafungamano kuendana na kiwango cha kimataifa na kuhimiza kiwango cha juu zaidi cha ufunguaji mlango

    Eneo la mtiririko wa Mto Changjiang ni moja kati ya maeneo yanayopata maendeleo makubwa zaidi ya kiuchumi, pia lina kiwango cha juu zaidi cha ufunguaji mlango, na uwezo mkubwa zaidi wa uvumbuzi. Pia linashika nafasi muhimu katika ujenzi wa kisasa wa taifa na muundo wa ufunguaji mlango wa pande zote. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Luo Wen anasema:

    "Eneo hilo litatafuta njia ya kubadilisha sifa yake ya kiikolojia kuwa sifa ya maendeleo ya uchumi na jamii, na kufanya uvumbuzi wa kimuundo wa mafungamano ya kanda hiyo ili kuelekeza maendeleo ya mafungamano ya eneo la mtiririko wa Mto Changjiang."

    Mji wa Shanghai ni mji muhimu kwenye eneo hilo. Naibu meya wa mji huo Bw. Chen Yin ameeleza kuwa, mji huo utaharakisha ujenzi wa vituo vya uchumi, fedha, biashara, uchukuzi wa majini na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, ili kufanya kazi ya kuongoza katika maendeleo ya eneo hilo. Anasema:

    "Tutaimarisha ushirikiano katika kuhimiza ufunguaji mlango wa kifedha katika maendeleo ya viwanda, kueneza mtandao wa miundombinu mipya ikiwemo 5G ili kuongeza uwezo wa utoaji wa huduma, na kuimarisha udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, na kuzidi kuboresha mazingira ya kiikolojia."

    Mkoa wa Anhui una nguvu kubwa ya kufanya uvumbuzi. Naibu mkuu wa mkoa huo Bw. Deng Xiangyang ameeleza kuwa, Anhui itafanya juhudi za kujenga kituo cha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia:

    "Tutaimarisha maendeleo ya pamoja ya utafiti wa kimsingi, matumizi na uvumbuzi wa teknolojia, kushirikiana na mji wa Shanghai, na mikoa ya Jiangsu na Zhejiang kukuza teknolojia muhimu, ili kupata maendeleo mapya kwa msukumo wa uvumbuzi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako