• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shujaa yajikwaa ikianza kampeni ya Raga ya Dunia mjini Dubai

  (GMT+08:00) 2019-12-06 18:10:58

  Timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande ya Kenya almaarufu Shujaa imefungua kampeni yake ya Mashindano ya Raga ya Dunia msimu wa 2019-2020 kwa kichapo cha alama 17-12 dhidi ya Afrika Kusini kwenye duru ya Dubai Sevens, Alhamisi. Shujaa iliongoza 12-5 wakati wa mapumziko kupitia miguso ya Alvin Otieno na Vincent Onyala, huku Daniel Taabu akaongeza mkwaju wa mguso wa Otieno. Hata hivyo, moto wa Shujaa ulizimwa kabisa na Afrika Kusini iliyorejea kwa nguvu na bidii kubwa katika kipindi cha pili. Katika kipindi hiki, Kenya, ambayo inanolewa na kocha Paul Feeney kutoka New Zealand, haikufunga alama, huku Afrika Kusini ikipachika alama za ushindi kupitia miguso ya Rosko Specman na Seabelo Senatla na mkwaju kutoka kwa Justin Geduld.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako