• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka Marekani kutozuia tena mapambano dhidi ya ugaidi duniani

    (GMT+08:00) 2019-12-06 18:53:28

    Shirika Kuu ya Utangazaji la China (CMG) limetoa makala ikisema, kitendo cha baraza la chini la bunge la Marekani kupitisha mswada kuhusu sera ya haki za binadamu ya wauygur ya mwaka 2019, kimeonyesha vigezo viwili vya Marekani juu ya suala la kupambana na ugaidi na kuharibu ushirikiano wa kupambana na ugaidi duniani.

    Pia kitendo hicho kimeonyesha madhumuni ya Marekani kuingilia mambo ya ndani ya China kwa kutumia kisingizio cha "haki za binadamu", kitendo ambacho kimepingwa kithabiti na watu wote wa China na jumuiya ya kimataifa. Makala hiyo imesema, katika miaka ya karibuni, Marekani imekiuka haki za binadamu na kuhimiza umwamba wake kwa kutumia kisingizo cha "haki za binadamu".

    Makala hiyo imesisitiza kuwa, suala la Xinjiang si suala la kikabila, kidini au haki za binadamu, bali ni suala la kupambana na ugaidi na kupinga kufarakanisha taifa. China inaitaka Marekani kuacha kuingilia mambo ya ndani ya China kwa kutumia suala la Xinjiang, na kuacha vigezo viwili katika kupambana na ugaidi mkali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako