• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutotumia vizuri ziwa Victoria kwaiponza EAC

    (GMT+08:00) 2019-12-06 19:19:39
    Kutotumia usafiri wa majini kwa ziwa Victoria ipasavyo kumeisababishia jumuiya ya Afrika mashariki hasara kubwa sana ya dola bilioni 60 kila mwaka. Ziwa Victoria linazifaidi nchi za Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda. Hata hivyo, inakisiwa kwamba mataifa haya yamekuwa yakikusanya dola bilioni sita kutoka kwa usafiri na shughuli zingine za majini kwenye ziwa Victoria. Haiya yalibainika kwenye kongamano la pamoja la mawaziri la mikakati kuhusu usafiri wa majini kwenye Ziwa Victoria. Mkutano huu uliandaliwa Kampala, nchini Uganda. Nchini Uganda, usafiri na shughuli zingine katika ziwa Victoria zimeathirika pakubwa kw miaka 35 kutokana na mafuriko. Hali kadhalika miundo msingi mibovu. Nchini Kenya, magugu maji yanayoota ndani ya ziwa hili, yamezidi kulemaza shughuli za kila siku kwenye Ziwa Victoria. Hivyo, ipo haja kwa mataifa ya Afrika Mashari yanayofaidika na ziwa Victoria, kuwajibika zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako