Awali, ripoti zilienezwa mitandaoni kuwa KRA ilikuwa imeafikia uamuzi wa kutoza ushuru wa mahari baada ya kushindwa kutimiza kiwango cha ushuru ilichohitajika kukusanya.
Baadhi ya Wakenya walifahamisha mamlaka hiyo kwamba vijana tayari wamelemewa na maisha, na hivyo hawakuhitaji mzigo mwingine wa ushuru.
Hata hivyo kuna wengine waliosisitiza kwamba KRA ilikuwa kweli imetoa tangazo hilo, lakini ikabadili nia haraka baada ya kuona hisia za Wakenya. Kwa uhalisia, inaweza kuwa vigumu kwa KRA kutoza ushuru wa mahari, ikizingatiwa kuwa wanaooana hawana mitambo ya kielektroniki (ETR), ambayo hutumika kuweka ithibati ya malipo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |