• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 30-Desemba 6)

    (GMT+08:00) 2019-12-06 20:54:15

    Wahamiaji 58 wafa maji baada ya boti kuzama

    Zaidi ya wahamiaji hamsini na nane wamekufa maji baada ya boti walilokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Mauritania. Walikuwa wahamiaji 150 na walikuwa wakitokea Gambia katika boti kabla ya boti hiyo kuzama Jumatano jioni wiki hii.

    Miili hamsini na nane imepatikana wakati huu na wahamiaji 85 wameokolewa. Kulingana na manusura, boti hiyo iliondoka Gambia Novemba 27 ikielekea Uhispania.

    Njia hiyo iliwahi kutumiwa katika siku za nyuma, na hivi wahamiaji wameanza sasa kuitumia. Yote hayo huenda ni kutokana na usalama kuimarika katika bahari ya Mediterranian. Wanaosafirisha wahamiaji hao hufanya waachotaka ili mradi tu wapate fedha.Wanajaribu kutumia njia yoyote ile kwa kuwasafirisha wahamiaji wanaotaka kiuingia Ulaya. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) imesema abiria 83 wameweza kuogelea hadi nchi kavu. Mkuu wa ujumbe wa IOM nchini Mauritania Laura Lungarotti, amesema mamlaka ya Mauritania inashirikiana vyema na ofisi hiyo.


    1  2  3  4  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako