• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu watatu wauawa kwenye shambulizi la kufyatua risasi katika kituo cha jeshi la anga cha Pensacola, Marekani

  (GMT+08:00) 2019-12-07 17:11:31

  Takriban watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mshambuliaji kufyatua risasi kwenye jengo la darasa katika kituo cha jeshi la Anga huko Pensacola, nchini Marekani.

  Kamanda mkuu wa polisi wa kaunti ya Escambia David Morgan amesema manaibu kamanda wawili walimkabili mshambuliaji na kumuua, na kwamba maofisa hao wawili pia wamepigwa risasi, lakini wanatarajiwa kupona baada ya kupatiwa matibabu. Maofisa wengine wawili waliojeruhiwa kwa risasi wamepelekwa hospitali ambapo mmoja amefariki. Katika mkutano na wanahabari gavana wa Florida Ron DeSantis amedokeza kuwa mshambuliaji ni askari wa Saudia. Na mamlaka za Marekani sasa zinaangalia kama mshambuliaji anahusiana na ugaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako