• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xinjiang yaondoa ugaidi kwa kuimarisha utulivu na ustawi

    (GMT+08:00) 2019-12-07 17:14:15

    Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani limetoa Mswada wa mwaka 2019 wa Sera ya Haki za Binadamu za Wauyghur, na kupaka matope sera ya serikali ya China katika mkoa wa Xinjiang. Kitendo hicho kimelaumiwa vikali na serikali ya China pamoja na  wakazi wa makabila mbalimbali mkoani Xinjiang. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "Xinjiang yaondoa ugaidi kwa kuimarisha utulivu na ustawi."

    Tahariri hiyo inasema tangu miaka ya 90 ya karne iliyopita, magaidi, wafarakanishaji, na watu wenye msimamo mkali wa kidini wamezusha maelfu ya mashambulizi ya kigaidi mkoani Xinjiang, na mashambulizi hayo yalivuruga utaratibu wa jamii na kukiuka haki za binadamu za wakazi wa mkoa huo. Ili kupambana na ugaidi, serikali ya China ilichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuanzisha vituo vya mafunzo ya ufundi stadi, ili kuwasaidia watu walioathiriwa na ugaidi na msimamo mkali kupata uwezo wa kuendesha maisha.

    Kutokana na juhudi hizo zenye ufanisi, kwa miaka mitatu mfululizo hakuna shambulizi la kigaidi lililotokea mkoani Xinjiang, na hali hii imehakikisha usalama wa wakazi wa makabila mbalimbali, na pia imeleta mazingira mazuri kwa maendeleo ya uchumi na jamii mkoani humo.

    Hivi sasa mkoa wa Xinjiang una ustawi usiopatikana katika historia yake. licha ya upande wa sababu ya mfumuko wa bei, pato la mkoa huo kwa mwaka jana liliongezeka kwa mara 200 ikilinganishwa na mwaka 1952, na katika miaka 30 iliyopita, wastani wa pato la wakazi wa Xinjiang umeongezeka kwa zaidi ya mara 100.

    Utulivu na ustawi wa mkoa wa Xinjiang haupatikani kwa urahisi, na hali nzuri ya hivi sasa haipaswi kuharibiwa na nguvu yoyote. Hivyo China hairuhusu nchi yoyote kuingilia kati mambo ya Xinjiang, na kusumbua hatua za China za kupambana na ugaidi na kuendeleza uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako