• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya watu waliokufa kwenye ajali ya moto Delhi India yafikia 43

  (GMT+08:00) 2019-12-08 17:19:27

  Idadi ya watu waliokufa katika ajali ya moto iliyotokea leo asubuhi mjini Delhi, India imefikia 43. Moto huo ulizuka nje ya jengo la ghorofa nne katika eneo la kaskazini la Filimistan mjini Delhi

  Shuhuda mmoja amesema chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme. Wengi wa waliokufa kwenye ajali hiyo ni wafanyakazi vibarua wahamiaji kutoka jimbo la mashariki la Bihar, na wakati moto unazuka walikuwa wamelala.

  Ofisa wa idara ya zimamoto amesema walifika kwa wakati kwenye eneo la tukio, lakini lango lilifungwa na walishindwa kuingia ndani, na watu walikuwa wakipiga kelele kuomba msaada. Baada ya kuvunja mlango na kuingia walifanikiwa kuwaokoa watu , ambao wengi wamepoteza fahamu kutokana na kuvuta moshi wenye sumu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako