• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jumuiya ya kimataifa yalaani Marekani kwa kupitisha mswada kuhusu hali ya Xinjiang

  (GMT+08:00) 2019-12-08 18:15:28

  Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani hivi karibuni limepitisha "mswada wa mwaka 2019 wa sera ya haki za binadamu za Wauyghur". Jumuiya ya kimataifa inaona kitendo hiki kinaingilia kati mambo ya ndani ya China, na kuipaka matope China katika juhudi zake za kuondoa ugaidi.

  Wizara ya mambo ya nje ya Syria imesema, serikali ya China ina haki ya kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi yake, na pia imetoa mchango katika shughuli za kupambana na ugaidi duniani.

  Profesa Stephen Ndegwa wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani, amesema mswada huo unaingilia kati mambo ya ndani ya China, na serikali ya China haipaswi kulaumiwa kwa hatua yake ya kupambana na ugaidi.

  Mtaalamu wa mambo ya China wa Ufaransa Bibi Sonia Bressler amesema mswada huo umeonesha umwamba wa Marekani, na haki za binadamu ni kisingizio cha Marekani kupotosha ukweli wa mambo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako