• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • "Kufumbia kwa makusudi" ni kitendo kinachohujumu ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi

  (GMT+08:00) 2019-12-09 08:59:27

  Hivi karibuni Kituo cha televisheni cha CGTN kilicho chini ya Shirika kuu la utangazaji la China CMG kimetangaza filamu za documentary kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi mkoani Xinjiang, ambazo zimeonesha vitendo vya kikatili vilivyofanywa na magaidi na watu wenye itikadi kali ya kidini mkoani Xinjiang, na kufafanua kwa kina juhudi zinazofanywa na China kuondoa matatizo yaliyopo.

  Vyombo vya habari na wanasiaisa wa nchi za magharibi ambao siku zote wanatumia vigezo viwili kwenye suala la kupambana na ugaidi, "wamefumbia kwa makusudi na kukaa kimya" mbele ya ukweli uliorekodiwa na kuoneshwa wazi kwenye filamu hizo.

  Ugaidi na itikadi kali ni maadui wa binadamu wote, na pia ni changamoto ya kiusalama inayoikabili jumuiya ya kimataifa, ambapo hakuna nchi yoyote inayoweza peke yake kujiepusha na suala hilo. Ripoti inaonesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018, matukio 639 ya kigaidi yalitokea katika nchi 42 duniani.

  Lakini wanasiasa wa nchi za magharibi ambao hawajali hata kidogo hali halisi ya mkoani Xinjiang, siku zote wanatumia visingizo vya "haki za binadamu" na "demokrasia" na kupaka matope sera ya China kuhusu mkoa wake wa Xinjiang, kwa lengo la kuifarakanisha na kuivuruga China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako