• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Leicester City yazidi kupaa juu baada ya kuinyeshea mvua ya magoli 4-1 Aston Villana

  (GMT+08:00) 2019-12-09 09:21:46

  Jamie Vardy ametingisha wavu mara mbili huku Leicester City ikiirambisha mchanga Aston Villana kwa 4-1 na kuweka rikodi ya klabu kwa kushinda mechi 8 mfululizo za Premier League na kuzidi kuwa na matumaini ya kuwafikia vinara Liverpool. Upande wa Brendan Rodgers kwa mara nyingine ulipunguza pengo la kufikia nafasi ya juu kwa alama nane katika mchezo safi uliogaragazwa huko Villa Park, ambao umemshuhudia mshambuliaji wa zamani wa England Vardy akichana wavu katika mchezo wa nane mfululizo. Vardy alitupiwa pasi na Kelechi Iheanacho na kufungua njia ya magoli katika dakika ya 20. Leicester ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, lakini sasa ina faida ya pointi sita dhidi ya Manchester City baada ya upande wa Pep Guardiola kushindwa na Manchester United Jumamosi .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako