• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namibia yachukua hatua za kuimarisha uchumi baada ya Moody's kushusha hadhi ya uchumi wake

    (GMT+08:00) 2019-12-09 09:30:35

    Serikali ya Namibia imetangaza kuchukua hatua za kuimarisha uchumi kufuatia Shirika la wawekezaji la Moody's kushusha hadhi ya uchumi wake mwishoni mwa wiki hii.

    Waziri wa Fedha wa Namibia Bw. Calle Schlettwein ametoa taarifa kuwa kutokana na changamoto za mazingira za kiuchumi, kushusha kwa hadhi ya uchumi kulitarajiwa, na amesisitiza haja ya kutafuta njia za kuboresha uchumi ambao umekuwa ukipungua kwa miaka miwili iliyopita.

    Bw. Schlettwein ameongeza kuwa serikali inajitahidi kuimarisha ukuaji wa uchumi na kutelekeza mabadiliko ya sera ya kimuundo ili kusaidia shughuli za uchumi, kuboresha biashara, dhamana ya sera na kuleta ufufuaji wa kiuchumi na usimamizi endelevu wa deni la umma.

    Aidha amesema serikali ya Namibia inashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa utekelezaji wa mipango ya mikopo ya dola za kimarekani milioni 274 katika miaka mitatu ijayo katika sekta ya kilimo, reli na miundombinu ya barabara, usafiri wa umma na elimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako