• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Wanaokwepa kulipa ushuru matatani

  (GMT+08:00) 2019-12-09 18:54:05
  Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya KRA, imeanza mikakati ya kuwasaka na kuwachukulia hatua kali mabwanyeye na kampunzi zinazokwepa kulipa ushuru. KRA sasa itaanza kuchukuwa mali, mishahara na kufuatilia akaunti za benki za wote wanaokwepa kulipa ushuru.

  Hii ni mojawapo ya hatua kali ambazo KRA imewahi kuchukuwa katika utendakazi wake, ili kuhakikisha kwamba inaafikia malengo yake ya kukusanya ushuru. Tayari KRA imeorodhesha majina ya kampuni na matajiri ambao inasemekana wanadaiwa pesa nyingi sana.

  Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya inapania kukusanya shilingi bilioni 20 kupitia mali na mishahara ya wote ambao wamekuwa wakikwepa kulipa ushuru.

  Baadhi ya bidhaa itakayochukuliwa ni pamoja na magari, mashamba,majumba, afisi pamoja na vifaa vilivyomo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako