• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: TBS yawashauri wafanyibiashara

  (GMT+08:00) 2019-12-09 18:54:35
  Wadau wamekutana katika mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji wamepatiwa elimu kuhusiana na majukumu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), fursa ya wajasiriamali kupatiwa bure alama ya ubora pamoja na kuzipatia ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.

  Mikutano hiyo ya mashauriano kwa mikoa ya Kanda ya Pwani iliyoanza Desemba 4, mwaka huu na kuhudhuriwa na Mawaziri na Manaibu Waziri takribani 13 ni mwendelezo wa mikutano iliyotangulia inayolenga kuzipatia ufumbuzi changamoto za zinaziwakabili wafanyabiasha na wawekezaji. Mikoa hiyo ya Kanda ya Mashariki ni Morogoro, Pwani wenyewe na mikutano hiyo ilihitimishwa jijini Dar es Salaam.

  Katika mikutano Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya, aliwapatia elimu wadau hao kuhusu fursa wanazopata wafanyabiashara na wazalishaji ambao bidhaa zao zimekidhi viwango vya ubora, kuhamasisha wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bure pamoja na kuzipatia majibu changamoto wanazokumbana wadau wake mbalimbali.

  Dkt. Ngenya alitaja fursa zinazotolewa na shirika hilo kwa wajasiriamali ambazo ni pamoja kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozalisha bila malipo kwa miaka mitatu lengo likiwa ni kuwawezesha kupanua soko la bidhaa zao na kuwaondolea vikwazo vya kibiashara.

  Alisema Serikali imeanzisha utaratibu huo ili kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa zenye ubora na kupanua wigo wa masoko hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako