• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yahimiza Marekani kuacha kutafuta maaduni

  (GMT+08:00) 2019-12-09 19:18:35

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inashauri Marekani kuacha mawazo ya kurudisha vita baridi iliyopitwa na wakati na kutoendelea kutafuta maadui.

  Habari zinasema, hivi karibuni, wakati akihutubia, waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. Mark Esper alisema, ingawa tishio la usalama la Mashariki ya Kati limeongezeka, lakini ataendelea kubadilisha msingi wa maendeleo ya jeshi la Marekani kuwa kushindana na majeshi ya China na Russia.

  Bibi Hua amesema, bajeti ya kijeshi ya Marekani ya mwaka huu, imefikia dola za Marekani bilioni 716 ambayo imechukua zaidi ya asilimia 40 ya matumizi yote ya kijeshi duniani. Pia idadi hiyo ni sawa na matumizi ya kijeshi ya jumla ya nchi za nafasi ya 2 hadi 10..

  "Marekani ina mamia ya vituo vya kijeshi duniani. Katika miaka 240 hivi tangu kuanzishwa kwa taifa hilo, ni miaka 16 tu haikuwa na vita. Marekani inalazimisha nchi nyingine kubadilisha utawala, kuchochea 'mapinduzi ya rangi', kushinikiza ovyo nchi nyingine, na kusababisha vurugu na matatizo ya maisha ya watu katika sehemu mbalimbali, zikiwemo Iraq, Afghanistan, Syria, na Venezuela. "

  Bibi Hua pia amesisitiza kuwa, maendeleo ya nguvu ya ulinzi wa taifa ya China yanalenga kulinda umoja wa taifa, ukamilifu wa ardhi na maslahi ya maendeleo. Pia yanakidhi mahitaji ya kulinda amani na utulivu wa kimataifa na kikanda.

  Kuhusu ripoti zilizotolewa na mashirika ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa kuhusu Marekani na baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya kukiuka haki za binadamu, Bibi Hua amesema, katika siku za karibuni, haki za binadamu nchini Marekani na baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya zinaendelea kuzorota, pengo kati ya watu maskani na matajiri kuendelea kuwa kubwa, na masuala ya ubaguzi wa rangi yamekuwa mbaya zaidi. Bibi Hua amesisitiza,

  "Kazi ya kulinda haki za binadamu si maneno matupu. Pia haipaswi kuwa kisingizio cha kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine. Tunataka Marekani itimize ahadi zake za haki za binadamu, kuhakikisha maslahi ya kimsingi ya makundi yote hasa makundi maalum ili kutoa mchango halisi kwa maendeleo ya haki za binadamu nchini humo na duniani."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako